Kwa mujibu wa mtandao wa habari wa Arab Online, akizungumza na waandishi habari mjini Berlin, Heide Simonis amesema: “Hata baada ya kupita wiki mbili baada ya kutangazwa usitishwaji vita Ukanda wa Gaza na jitihada za taasisi za kimataifa kuboresha hali ya eneo hilo, watoto wanaishi maisha magumu na ya kusikitisha katika ukanda huo”.
Ametoa wito kwa jumuiya za kimataifa kutuma haraka misaada ya kibinadamu huko Gaza ili kuwaondolea watoto masaibu na hali ngumu ya maisha.
Heide Simonis ameongeza kuwa: “Licha ya usitishwaji vita wa muda Ukanda wa Gaza, watoto wa eneo hilo wamekuwa wakisubiri kwa muda mrefu misaada ya kibinadamu kuwafikia. Hii ni katika hali ambayo wakati wa hujuma ya Israel dhidi ya eneo hilo walikuwa wakipata misaada ya kimataifa kwa kasi zaidi”.
Mkurugenzi wa tawi la Ujerumani la UNICEF amemaliza kwa kusema kwa kwa kutoa wito wa kuheshimiwa ubinadamu wa wakazi wa Gaza, kufunguliwa vivuko vyote vya eneo hilo na kurahisisha ufikaji wa misaada ya kibinadamu kwa wakazi wasio na ulinzi wa ardhi hiyo ya Palestina. 356830