IQNA

Kikao cha fasihi ya Kiislamu chafanyika nchini India

11:33 - February 02, 2009
Habari ID: 1738763
Kikao cha cha nane cha fasihi ya Kiislamu kilifanyika jana Jumapili huko katika mji wa Bhopal nchini India.
Kwa mujibu wa tovuti ya Indianmuslims, kikao hicho ambacho kimeandaliwa na Baraza la Fasihi ya Kiislamu la India kimewajumuisha wahadhiri wa vyuo vikuu pamoja na wahadhiri na vilevile walimu wa shule mashuhuri za Kiislamu nchini India.
Lengo la kufanyika kikao hicho limetajwa kuwa ni kueneza fasihi yenye thamani kubwa ya Kiislamu kwa ajili ya kuwaongoza wanadamu na kuimarisha uelewa na muamko wao katika kukabiliana na masuala yasiyo na thamani kubwa katika maisha yao, masuala ambayo yameenea kote duniani.
Uchunguzi wa historia ya fasihi ya Kiislamu, athari na kazi za fasihi za wanazuoni wa Kiislamu pamoja na kuarifishwa vituo vya fasihi na shughuli zao ni miongoni mwa sababu zilizopelekea kufanyika kikao hicho. 357256
captcha