IQNA

Kikao cha Ujenzi Mpya wa Gaza chafanyika Qatar

9:21 - February 03, 2009
Habari ID: 1739331
Kikao cha taasisi zisizo za kiserikali cha kujadili njia za ujenzi mpya wa Gaza kimefanyika Doha mji mkuu wa Qatar.
Kwa mujibu wa gazeti la Peninsula, kikao hicho kilihudhuriwa na wawakilishi wa mashirika yasiyo ya kiserikali kutoa nchi 30 duniani. Washiriki walijadili njia za kujenga upya maeneo ya Ukanda wa Gaza yaliyoharibiwa katika vita vya siku 22 vya Wazayuni na vile vile njia za kuwafikishia misaada raia wanaopata masaibu Gaza.
Hany al-Bana, Mkuu wa Jumuiya ya Misaada ya Kibinadamu ya Shirika la Kimataifa la Misaada ya Kiisalmu amehutubia kikao hicho na kutoa wito kwa mashirika yasiyo ya kiserikali kote duniani kusaidia ujenzi mpya wa Gaza.
Naye Nadia Evans kutoka Idara ya Ushirikiano wa Masuala ya Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa (UNOCHA) ameelezea umuhimu wa kuzidishwa ushirikiano kwa ajili ya ujenzi mpya wa Gaza. Amesema, hivi sasa kuna mashirika 50 yasiyo ya serikali kutoka nchi mbalimbali duniani na idara 15 za Umoja wa Mataifa zinazohusika na huduma za misaada huko Gaza.
Washiriki katika kikao cha Doha vile vile wamejadili masuala kama vile nafasi ya vyombo vya habari katika kuwasaidia watu wa Gaza. Wamesema, vyombo vya habari vinaweza kutumika kwa ajili ya kuwapasha watu habari kuhusu hali halisi ya Uakanda wa Gaza. 358036
captcha