Kwa mujibu wa toleo la Februari Mosi la gazeti la Al Dastur la Jordan, Wail Al Saqa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wahandisi wa Jordan ameashiria azma ya taasisi nyingi duniani kusaidia Gaza na kusema kuwa: "Jumuiya hiyo itapokea tu misaada ya mashirika ya kiraia na yasiyo na kiserikali.
Akizungumza katika kikao cha waandishi habari kilichofanyika huko Amman na kuhudhuriwa pia na Osama Abdulhalim Al Essawi, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wahandisi wa Palestina, al Saqa ameongeza kuwa: " Hadi sasa wanaharakati kutoka Indonesia, Malaysia na Uturuki wametangaza kushiriki katika jumuiya hiyo na wamesema wako tayari kutuma misaada Gaza kupitia Jordan".
Wail al Saqa vile vile ameashiria hujuma ya kinyama ya Wazayuni huko Gaza na kusema: "Wazayuni walilenga kwa makusudi taasisi muhimu za miundombinu za Gaza pamoja na nyumba za raia ili kwa njia hiyo Wapalestina wakabiliwe na masaibu na hali ngumu ya maisha", 358155