IQNA

Mashindano ya Qur'ani nchini Bahrain

13:56 - February 03, 2009
Habari ID: 1739564
Mashindano ya 22 ya kitaifa ya Abdul Aziz bin Muhammad Aal Khalifa nchini Bahrain yamepangwa kufanyika mwezi Aprili huko Manama, mji mkuu wa nchi hiyo.
Gazeti la Bahrain la al-Waqt limeandika kwamba, mashindano hayo ambayo yatasimamiwa na Abdullah bin Khalid Aal Khalifa, mkuu wa Baraza Kuu la Masuala ya Kiislamu la Bahrain, yatafanyika katika sehemu mbili za kusoma na kuhifdhi Qur'ani Tukufu.
Muhammad al-Mahdi, katibu wa mashindano hayo ya mwaka huu amesema kuhusiana na suala hilo kwamba, wahifadhi na wasomaji Qur'ani wa Bahrain wana muhula wa kufikia tarehe 13 Aprili kusajili majina yao kwa lengo la kushiriki katika mashindano hayo. Amesema, mashindano hayo yataanza rasmi Jumatatu tarehe 20 Aprili.
Mashindano hayo ambayo yamepewa jina la marehemu Abdul Aziz bin Muhammad Aal Khalifa, mwalimu mashuhuri wa Qur'ani na mkurugenzi wa zamani katika Wizara ya Elimu na Malezi ya Bahrain, yataendeshwa na kamati maalumu ya marefa mashuhuri wa Qur'ani kutoka nchi hiyo. 357968
captcha