Kwa mujibu wa Mwambata wa Utamaduni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran mjini Khartoum, Hujjatul Islam Ansari, sherehe hiyo ya mjini Omdurman imehudhuriwa na idadi kubwa ya mashekhe wa kisufi, wahadhiri wa vyuo vikuu na wanachuo wa kitivo cha Kiislamu cha Chuo Kikuu cha Sudan.
Wazungmzaji katika sherehe hiyo wamejadili kadhia ya umoja, mshikamano na istikama ya aina yake ya taifa la Kiislamu la Iran tangu mwanzo wa harakati za Mapinduzi ya Kiislamu katika kukabiliana na utawala uliokuwa umejizatiti kwa silaha za Mfalme Shah. Aidha wametathmini miongozo na nasaha za Imam Khomeini (MA) ambazo zilipelekea kupatikana ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu.
Aidha washiriki wamejadili suala la ustawi na mafanikio ya mfumo wa Kiislamu wa Iran katika nyanja mbalimbali za kisayansi, kiviwanda, kijeshi, kielimu, kisheria, kiafya n.k katika kipindi cha miaka 30 iliyopita.
Mwishoni mwa sherehe hiyo kulifanyika mashindano yenye maudhui ya “Miaka 30 pamoja na Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran” na washindi watano walizawadiwa. 358991