Kwa mujibu wa mwadishi wetu mjini Mash'had, nuskha hiyo iiliyoandikwa kwa hati za kaligrafia za Naskh, imefasiriwa na ina maelezo yaliyoandikwa kwa hati za Nastalikh. Tarehe iliyosajiliwa katika nuskha hiyo ya Qur'ani ni karne ya 13 Hijria Qamariya.
Msahafu huo una kurasa 187 na ina ukubwba wa sentimeta 29 kwa 18.7.
Katika ukurasa wa kwanza wa msahafu huo kuna majina ya sura, maelezo na mapambo ya dhahabu.
Kurasa nane za mwisho za msahafu huo zina dua inayosomwa baada ya kumaliza kuisoma Qur'ani.
Msahafu huo ulizawadiwa Maktaba ya Astan Quds Razawi na Akhtar Khadem Bash mke wa marehemu Ali Mashar mwana wa Khan Baba Mashar. 359486