Muhammad Reza Wasifi, Katibu wa Duru ya 16 ya Zawadi ya Kimataifa ya Kitabu Bora cha Mwaka katika Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameongeza kuwa: “Katika duru hii ya zawadi ya kitabu bora zaidi duniani kwa mwaka, kwa mara ya kwanza, kitabu bora ni kutoka Uturuki katika nyanja ya masomo ya Qur'ani na tafsiri. Vile vile katika uga wa lugha za Kijerumani na Kiingereza kazi bora zaidi zilizochaguliwa ni tafsiri ya Qur'ani kwa lugha ya Kijerumani pamoja na mjumuiko kamili wa tafsiri na sayansi ya Hadithi. Katika uga wa lugha ya Kifaransa aidha kitabu kuhusu masomo ya Qur'ani kimechukua nafasi ya kwanza”.
Ameongeza kuwa: “Kwa hivyo nyanja za masomo ya Qur'ani mbali na kuwa na athari nyingi zilizowaisilishwa, vilevile kwa mtazamo wa lugha zimepiga hatua kuliko huko nyuma.
Duru ya 16 za Zawadi ya Kimataifa ya Kitabu Bora cha Mwaka imekuwa na vitabu vitatu bora katika sayansi za Qur'ani vinazojumuisha juzuu kadhaa”.
Mkurugenzi Mkuu wa Jumuiya na Shughuli za Kiutamaduni katika Wizara ya Utamaduni na Muongozo wa Kiislamu ya Iran amesema kuwa: “Sekta ya shughuli za Qur'ani imepewa umuhimu mkubwa katika duru hii ya 16 za Zawadi ya Kimataifa ya Kitabu Bora cha Mwaka. 359310