IQNA

Najaf yakamalisha maandalizi ya Msafara wa Mazishi ya Shahidi Ayatullah Khamenei

14:15 - July 06, 2026
Habari ID: 3482448
IQNA- Mamlaka katika Jimbo la Najaf nchini Iraq zimekamilisha maandalizi ya usalama, vifaa, na huduma kwa ajili ya msafara wa mazishi ya Kiongozi Shahidi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Seyed Ali Khamenei.

Gavana wa Najaf, Youssef Makki Kanawi, ametangaza kuwa shughuli za kumuaga Kiongozi Shahidi zitajumuisha programu mbili kuu. Ya kwanza ni hafla rasmi itakayofanyika Jumanne katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Najaf, ambapo viongozi wa ngazi ya juu wa Iraq watahudhuria, wakiwemo wakuu wa mihimili ya dola ya utendaji, sheria, na mahakama, viongozi wa kisiasa, wabunge, na wageni wengine mashuhuri.

Tukio la pili, ambalo ni msafara wa hadhara, limepangwa kuanza saa 12:00 asubuhi siku ya Jumatano, kuanzia kwenye daraja la juu lililoko karibu na Hospitali ya Al-Sadr kwenye Barabara ya Uwanja wa Ndege. Msafara huo utapita katika mji wa kale wa Najaf kabla ya kuhitimishwa katika Haram tukufu ya Imam Ali (AS).

Kanawi alieleza kuwa wawakilishi kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu wa Iraq, Kamandi ya Pamoja ya Operesheni, Vikosi vya Kujitolea vya Wananchi (PMU/Al-Hashd al-Shaabi), na Balozi wa Iran wamekamilisha mipango yote ya mwisho. Ameongeza kuwa Najaf imejipanga kikamilifu kuandaa “tukio la kihistoria.”

Mwili wa Kiongozi huyo shahidi wa Iran utazikwa kando ya Haram ya Imam Ridha (AS) siku ya Alhamisi, kufuatia misafara ya mazishi iliyofanyika Tehran, Qom, Karbala, na  Najaf. Mazishi hayo katika mji mtakatifu wa Mashhad yataashiria hatua ya mwisho ya mfululizo wa hafla za kitaifa za maombolezo nchini Iran na Iraq.

3498115

Habari zinazohusiana
captcha