IQNA

Mufti Mkuu wa Tunisia Asifu Urithi wa Mashahidi wa Ayatullah Khamenei katika Kuleta Umoja wa Kiislamu

12:04 - July 06, 2026
Habari ID: 3482447
IQNA – Mufti Mkuu wa Tunisia, Sheikh Hisham Ben Mahmoud, ametoa heshima zake kwa kiongozi shujaa wa Mapinduzi ya Kiislamu, Shahidi Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, akielezea mwito wake wake  kuhimiza umoja , mshikamano, na uvumilivu miongoni mwa Waislamu kama mwendelezo wa ujumbe wa Mtume Muhammad (SAW).

Akizungumza wakati huu wa majonzi makubwa kwa Ummah wa Kiislamu, Sheikh Ben Mahmoud alisema kuwa mwito wa kudumu wa Ayatullah Khamenei wa kutaka Waislamu wawe kitu kimoja unasalia kuwa miongoni mwa urithi wake mkubwa zaidi na wa kudumu.

Mufti huyo amesema kuwa kiongozi huyo shahidi alikuwa akisisitiza mara kwa mara maadili ya upendo, mshikamano, na uvumilivu wa pamoja miongoni mwa Waislamu, akiongeza kuwa mbinu yake hiyo ilikuwa ikionyesha njia ile ile iliyoanzishwa na Mtume Muhammad (SAW) na kuendelezwa katika kipindi chote cha Mapinduzi ya Kiislamu.

Sheikh Ben Mahmoud amesisitiza kuwa dira ya Ayatullah Khamenei ya umoja wa Kiislamu inaendelea kuwa chemchemi ya hamasa na mwongozo kwa Waislamu kote duniani, ikikumbusha umuhimu wa kufanya kazi kwa pamoja kukabiliana na changamoto zinazoukabili ulimwengu wa Kiislamu.

Kauli hii ya Mufti Mkuu inakuja huku ulimwengu wa Kiislamu ukiendelea kutafakari juu ya mchango wa Ayatullah Khamenei katika kuimarisha misingi ya kidini na kijiopolitiki, huku kukiwa na wito unaozidi kuongezeka wa kuhifadhi na kuendeleza misingi hiyo ya umoja wa Ummah. Ayatullah Khamenei aliuawa shahidi Febrauri 28 sawa na 10 ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani katika hujuma ya kigaidi ya Marekani  na Israel katika siku ya kwanza ya vita vya tawala hizo mbili dhidi ya Iran. Vita hivyo viliendelea kwa siku 40 ambapo Marekani ililazimika kuomba usitishaji vita kutokana na hujuma za kulipiza kisasi za Iran dhidi ya ngome za kijeshi na kiuchumi za Marekani na Israel katika eneo lote la Asia Magharibi.

3498116

Habari zinazohusiana
captcha