Hafla hiyo ya kiroho ilifanyika katika Taasisi ya Mahd Qur’an mjini Tehran, kwa ushiriki wa walimu wa Qur’ani, maqari na mahafidhi.
Tukio hilo la kiibada lilianza asubuhi ya siku ya Tasua na kuendelea hadi asubuhi ya Ashura.
Kila mwaka katika mwezi wa Muharram, vikao hivi vya Qur'ani huandaliwa kwa kumbukumbu ya marehemu mwalimu mashuhuri wa Qur’ani, Seyed Mohammad Hassan Seif, ambaye alikuwa miongoni mwa waanzilishi na wahudumu wakubwa wa uga wa Qur’ani Tukufu.
Katika hafla hiyo, kundi la wabobezi wa Qur’ani, wasomaji, mahafidhi na wapenda maneno ya wahyi huendelea kusoma aya za Mwenyezi Mungu bila kukatiza, kwa lengo la kukamilisha usomaji wa Qur’ani yote katika muda wa mchana na usiku mmoja.
Ibada hii ya kiroho ni dhihirisho la uhusiano wa ndani na wa kina baina ya utamaduni wa Ashura na mafundisho ya Qur’ani Tukufu; uhusiano ambao ndani yake mapenzi kwa Ahlul-Bayt (AS) yanaambatana na kutafakari kalamu ya Mwenyezi Mungu, jambo linalojenga mazingira yaliyojaa umaanawi, ikhlasi na kujitolea kwa Bwana na Kiongozi wa Mashahidi, Imam Husayn (AS).
3497972