IQNA

Karbala yakaribisha ‘Msafiri wa Kwanza wa Arbaeen’ wa Mwaka Huu

16:47 - July 07, 2026
Habari ID: 3482454
IQNA – Mwili mtakatifu wa Shahidi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayed Ali Khamenei, utapelekwa katika maeneo matakatifu nchini Iraq kwa ajili ya ziara ya mwisho (ziara ya mazishi), tukio ambalo ni la kwanza la aina yake katika kipindi cha miaka 69.

Katika kujiandaa na ziyaa hiyo ya mazishi, Mkoa wa Karbala umeanza maandalizi kwa kuweka bango maalum lenye ujumbe wa “Karibu, Msafiri wa Kwanza wa Arbaeen wa Mwaka Huu,” kama njia ya kutoa heshima ya mwisho kwa Shahidi wa Mapinduzi.

Kitendo hiki kimefanyika huku maandalizi makubwa yakiwa yameanza kupokea msafara wa mazishi, kama ishara ya kuenzi kwa heshima kubwa kuwasili kwa kiongozi huyo aliyerejea kwa Mola wake (marhum) katika maeneo matakatifu ya Iraq.

Misafara ya mazishi nchini Iraq itafanyika katika miji mitakatifu ya Najaf na Karbala siku ya Jumatano.

Arbaeen, huadhimisha siku 40 baada ya Siku ya Ashura (tarehe 10 Muharram), ambayo huomboleza kuuawa kwa shahidi, Imam Hussein (AS), mjukuu wa Mtume Muhammad (SAW). Katika kalenda ya mwezi ya Kiislamu, siku hii huangukia tarehe 20 Safar. Misafara ya ziara ya Arbaeen huanza kabla ya tarehe hiyo.

3498135

Habari zinazohusiana
captcha