IQNA

Maombolezo ya Kiongozi Shahidi Ayatuah Khamenei yafanyika nchini Marekani

14:31 - July 06, 2026
Habari ID: 3482449
MAREKANI
IQNA-Wakati shughuli za mazishi na kuaga mwili wa Kiongozi Shahidi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, zikiendelea nchini Iran, Waislamu na wafuasi wake nchini Marekani wameungana kufanya ibada za maombolezo kufuatia kuondoka kwa kiongozi huyo.

Hafla hizo za maombolezo zimefanyika katika Msikiti wa Manassas uliopo Virginia, nje kidogo ya mji mkuu wa Washington, DC, siku ya Jumapili jioni. Tukio hilo lilihudhuriwa na Waislamu kutoka mataifa mbalimbali, waliofika kuonesha mshikamano wao katika wakati huu wa majonzi.

Ibada hiyo ilitawaliwa na hali ya kiroho iliyojaa huzuni na imani; mazingira ambayo yaliakisi uhusiano wa kina wa waliohudhuria na fikra za kidini, mafunzo ya Ahl-ul-Bayt (AS), na utamaduni wa Ashura, jambo ambalo lilikuwa dhahiri kwa kila mmoja aliyekuwepo.

Abolfazl Mehrabadi, Mkuu wa Ofisi ya Kulinda Maslahi ya Iran mjini Washington, naye alihudhuria shughuli hiyo muhimu.

Tukio hilo lilianza kwa kisomo cha aya za Qur’ani Tukufu, kikifuatiwa na  sehemu za hotuba za Kiongozi huyo shahidi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran, hotuba zilizosisitiza dhana ya uongozi wa mstari wa mbele, kusimama kidete katika njia ya haki, na maana halisi ya muqawama au mapambano.

Katika hotuba yake kwenye hafla hiyo, Hujjatul Islam Seyed Suleiman, msomi na kiongozi wa kidini wa Kishia kutoka Pakistan anayehudumu Marekani, alisisitiza nafasi ya watu wanaotembea katika njia ya Ahl-ul-Bayt (AS) kwa kurejelea dhana ya upinzani na shahada.

Akizungumzia kuondoka kwa Kiongozi huyo, alisema kuwa kama ilivyokuwa kwa Imam Hussein (AS), Ayatullah Khamenei alikuwa mstari wa mbele katika kutetea Uislamu. Msomi huyo alisisitiza umuhimu wa kusimama katika upande sahihi wa historia, akiongeza kuwa katika mazingira ya ulimwengu wa sasa, kiongozi wa aina hiyo ni nadra kuonekana katika jamii za Magharibi.

“Kuuawa Shahidi Ayatullah Khamenei imetufunza somo la uvumilivu na msimamo,” alisema Hujjatul Islam Suleiman, akihitimisha kwa kusema kuwa yeyote anayechagua njia ya Mwenyezi Mungu atafikia daraja za juu kabisa.

3498117

Habari zinazohusiana
captcha