IQNA

Afisa Mwandamizi wa Iran Asisitiza Wajibu wa Kuadhibu Wauaji wa Kiongozi Shahidi Ayatollah Khamenei

16:55 - July 07, 2026
Habari ID: 3482455
l
IQNA – Kuadhibiwa kwa wauaji wa Kiongozi Shahidi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, ni wajibu wa kimsingi wa mamlaka ya Jamhuri ya Kiislamu, amesema afisa mwandamizi wa serikali.

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Iran, Mohammad Reza Aref, ameongeza kuwa haki hiyo itatekelezwa kwa kutumia busara ya kistratijia.

Siku ya Jumatatu, Aref alitumia mtandao wa kijamii wa X kutoa jibu kwa wito wa taifa wa kutaka haki, wito uliotolewa na umati mkubwa wa waombolezaji wakati wa msafara wa mazishi ya Kiongozi huyo shahidi na wanafamilia wake, ambao walikufa shahidi katika shambulio la kigaidi lililofanywa na Marekani na utawala wa Kizayuni mnamo tarehe 28 Februari.

Alisema kuwa wito huo unaakisi takwa halali la watu wa Iran la kutaka uwajibikaji.

“Takwa la haki la taifa la kuadhibu wauaji, ambalo liliibuliwa wakati wa msafara wa mazishi ya kihistoria, ni ombi la kisheria na linaoana kikamilifu na kanuni za kimataifa za kujilinda.”

“Utekelezaji wa haki ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ya kuadhibu kikamilifu wahalifu wa uhalifu huu ni wajibu wa kimsingi wa dola (sovereign duty) ambao utatekelezwa kwa busara ya kistratijia.”

Mamilioni ya waombolezaji walikusanyika Tehran kwa ajili ya hafla za kihistoria za mazishi ya Kiongozi huyo shahidi, huku washiriki wengi wakitaka haki itendeke kwa kuadhibiwa waliohusika na mauaji hayo. Maafisa wanasema kuwa mkusanyiko huu wa umma ndio mkubwa zaidi katika historia ya kisasa ya Iran.

/3498127

Habari zinazohusiana
captcha