Msafara huo ulianza 12:00 asubuhi kwa saa za Iran (0230 GMT) Jumatatu, ukitokea katika eneo la Ukumbi wa Musallah mjini Tehran, ambapo mwili ulikuwa umewekwa kwa ajili ya kuagwa kwa siku mbili.
Waombolezaji wanatarajia msafara huo kudumu kwa saa 10 hadi 12, ukipita katika njia ya kilomita 10 kupitia Mtaa wa Damavand, Medani ya Imam Hussein, Mtaa wa Enqelab, Medani ya Enqelab, Mtaa wa Azadi, Medani Azadi, na Barabara kuu ya Shahid Lashgari, iliyo karibu na uwanja wa ndege wa Mehrabad.
Siku ya Jumapili, Ayatullah Jafar Sobhani aliongoza swala ya mazishi kwa Kiongozi huyo shahidi, mkwe wake Dkt. Mesbah-ul-Hoda Bagheri-Kani, Zahra Haddad-Adel ambaye ni mku wa Kiongozi Muadhamu wa Sasa Ayatullah Mujtaba Khamenei, mjukuu wake Zahra Mohammadi-Golpayegani (aliyekuwa na umri wa miezi 14), na binti yake, Seyyedeh Bushra Hosseini-Khamenei.
Ujumbe kutoka nchi nyingi, wakiwemo wakuu wa nchi, mawaziri wakuu, na maafisa wa ngazi ya juu kutoka Urusi, China, India, Pakistan, Iraq, Tajikistan, Uturuki, Tanzania na mataifa mengine kadhaa, walikuwa wamewasili Tehran siku ya Ijumaa kutoa heshima zao za mwisho.
Shughuli za mazishi zitaendelea kwa matukio kama hayo katika mji mtakatifu wa Qom siku ya Jumanne, yakifuatiwa na kisha katika maeneo matakatifu ya Imam Ali (AS) huko Najaf, na Imam Hussein (AS) pamoja na Hazrat Abbas (AS) huko Karbala siku ya Jumatano.
Mazishi yatafanyika siku ya Alhamisi, Julai 9, katika haram takatifu ya Imam Ridha (AS) huko Mashhad, kwa mujibu wa usia wa Kiongozi huyo aliyeuawa shahidi.
Imam Khamenei aliuawa shahidi Febrauri 28 sawa na 10 ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani katika hujuma ya kigaidi ya Marekani na Israel katika siku ya kwanza ya vita vya tawala hizo mbili dhidi ya Iran. Vita hivyo viliendelea kwa siku 40 ambapo Marekani ililazimika kuomba usitishaji vita kutokana na hujuma za kulipiza kisasi za Iran dhidi ya ngome za kijeshi na kiuchumi za Marekani na Israel katika eneo lote la Asia Magharibi.
3498116