IQNA

Hafla ya Kisomo cha Qur’ani Tukufu ya Ashura yafanyika Karbala

15:15 - June 27, 2026
Habari ID: 3482407
Ashura Qurani
IQNA – Hafla ya kisomo cha Qur’ani Tukufu imefanyika siku ya Ashura katika mji mtukufu wa Karbala.

Kwa mujibu wa taarifa ya Al-Kafeel, tukio hilo la Qur’ani limeandaliwa na Baraza la Kitaaluma la Qur’ani Tukufu, linalohusishwa na Ataba ya Hadhrat Abbas (AS).

Sheikh Jawad al-Nasrawi, mkurugenzi wa baraza hilo, amesema kuwa hafla hiyo imeandaliwa kwa ajili ya kuhuisha kumbukumbu ya siku ya Ashura kupitia usomaji wa Qur’ani Tukufu na kuwasilisha thawabu zake kwa Imam Hussein (AS), ahli zake na masahaba wake.

Ameongeza kuwa hafla hiyo ya usomaji wa Qur’ani imefanyika kwa ushiriki wa idadi kubwa ya waombolezaji, ambapo, kwa kufuata kielelezo cha Imam Hussein (AS) aliyekesha usiku wa kuamkia Ashura akisoma Neno la Mwenyezi Mungu, sehemu kadhaa za Qur’ani Tukufu zimesomwa.

Al-Nasrawi ameeleza kuwa programu hiyo ni miongoni mwa shughuli za kila mwaka zinazoandaliwa na Baraza la Kitaaluma la Qur’ani Tukufu, na kwamba lengo lake ni kuimarisha maadili na misingi ya Kiqur’ani ya Imam Hussein (AS), ambaye alijitoa mhanga yeye mwenyewe, familia yake na masahaba wake kwa ajili ya kuyasimamisha na kuyatetea.

3497987

captcha