IQNA

Maonyesho ya kimataifa ya Mfungamano na Gaza yafanyika Ugiriki

22:33 - February 08, 2009
Habari ID: 1741704
Maonyesho ya kimataifa ya "Mfugamano na Gaza" yamefanyika nchini Ugiriki na kuhudhuriwa na wasanii kutoka Cyprus, Lebanon na Ugiriki katika mji wa Salonic kaskazini mwa nchi hiyo.
Kwa mujibu wa mtandao wa habari wa Arab Online, wasanii washiriki katika maonyesho hayo walionyesha taswira za masaibu na matatizo ya Wapalestina katika Ukanda wa Gaza kufuatia hujuma ya kinyama ya Wazayuni iliyopelekea maelfu wa raia hasa wanawake na watoto kuuawa shahidi na kujeruhiwa.
Vile vile kulikuwa na picha za msikiti wa Al Aqsa, athari za kale za Kiislamu za Palestina na Quds Tukufu na, ukuta wa kibaguzi unaojengwa na Wazayuni katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.
Watazamaji katika maonyesho hayo walipewa vijitabu kuhusu historia ya Palestina na kukaliwa kwa mabavu ardhi hiyo na vikosi vya Kizayuni. Sanaa za mikono za Wapalestina pia zimeonyeshwa katika tukio hilo la kiutamaduni.
Ziyad A'antar msanii kutoka Lebanon aliyeshiri katika maonyesho hayo amesema, kuwapa himaya Wapalestina wasioweza kujilinda ni jambo la dharura na kunaweza kufanyika kwa njia mbalimbali. Amesema kuwa wasanii wanaweza kutumia taaluma yao kuonyesha jinai za Israel na matatizo ya Wapalestina. 360441

captcha