Mwenyekiti wa Muungano wa Mabaraza ya Kiislamu ya Australia Iqbal Patel amelaani vikali mashambulizi ya kinyama yaliyofanywa na Israel katika Ukanda wa Gaza na akasema: Kuna ushahidi wa kutosha wa kuthibitisha unyama uliofanywa na utawala ghasibu wa Israel dhidi ya raia wasiokuwa na hatia wa Palestina katika Ukanda wa Gaza.
Iqbal Patel ambaye tangu mwanzoni mwa mashambulizi ya Israel huko Gaza aliandika mengi kuthibitisha jinai za utawala huo, amesema kuwa mauaji ya idadi kubwa ya wanawake na watoto wadogo wa Gaza yanaonyesha taswira ya holocaust halisi katika eneo hilo.
Katika upande mwingine jumuiya za Kiyahudi za Australia zimepinga msimamo wa Waislamu wa nchi hiyo dhidi ya utawala wa Kizayuni wa Israel na kutangaza kwamba zitakata uhusiano wao na taasisi za Kiislamu iwapo hazitatupia mbali masimamo huo.
Waislamu waliowachache nchini Australia wamejibu vitisho hivyo vya jumuiya za Kiyahudi kwa kuunga mkono matamshi ya kupinga Uzayuni ya Iqbal Patel na msimamo wake dhidi ya Israel. 361163