Kwa mujibu wa gazeti la Qatar la al-Bayaan, washiriki wa kikao hicho cha siku tatu wametoa taarifa wakisisitiza umuhimu wa kuzinduliwa tovuti ya lugha za Kiafrika zitakazoshajiisha mitazamo ya wastani na masuala ya kuwakurubisha pamoja Waislamu.
Kwa mujibu wa gazeti hilo, washiriki wameitaka Jumuiya ya Kimataifa ya Uhubiri wa Kiislamu, Baraza la Kimataifa la Masuala ya Kheri ya Kiislamu na Jumuiya ya Masuala ya Kheri ya Qatar kufanya juhudi za kuanzisha masomo ya muda kwa maimamu wa misikiti na wahubiri vijana wa Kiislamu katika nchi za Kiislamu.
Washiriki wa kikao hicho pia wamesisitiza juu ya kuwepo umoja katika hotuba zinazotolewa na wahubiri pamoja na mahatibu wa Kiislamu na kutilia mkazo kwamba hutoba hizo zinapasa kutolewa kwa msingi wa kuwaunganisha Waislamu na stratejia ya kukurubisha pamoja madhehebu za Kiislamu.
Kikao hicho cha kimataifa ambacho kimewashirikisha maimamu wa misikiti ya nchi mbalimbali za dunia kilimalizika siku ya Jumanne nchini Sudan. 362461