Gazeti la al Sharq al Ausat linalochapishwa katika nchi kadhaa limeandika kuwa Ganiyev Ganov amesema, ameanza kusoma kitabu kitakatifu cha Waislamu ili kupata taswira na ufahamu huru kuhusu kitabu hicho.
Ganev amesema kuwa Qur'ani inakamilisha mwenendo wa Muislamu kwa kuathiri ada na tabia zake na kwamba hadi sasa hajapata ishara yoyoye ya kuhamasisha ugaidi na vitendo vya utumiaji mabavu katika aya za kitabu hicho kitakatifu.
Mwanasheria huyo wa Bulgaria ameashiria suala la kuwepo dini za aina tofauti katika mji mkuu wa nchi hiyo Sofia na akasema: Suala hilo linadhamini umoja wa taifa hilo na kwamba hitilafu katika mirengo ya kidini itakurubisha zaidi dini hizo.
Ganiyev amewahi kushika nyadhifa mbalimbali katika serikali ya Bulgaria na aliwahi kuwa mwakilishi katika bunge la nchi hiyo.
Zaidi ya Waislamu milioni moja wanaishi nchini Bulgaria. 365247