IQNA

Safari ya wabunge wa Uingereza katika Ukanda wa Gaza

18:26 - February 17, 2009
Habari ID: 1745367
Kundi la wabunge kumi wa Uingereza wanatarajia kufanya safari katika Ukanda wa Gaza hivi karibuni kwa lengo la kuchunguza kwa karibu hali mbaya ya ukanda huo kutokana na hujuma ya kijinai ya utawala wa Israel dhidi ya wakazi wasio na hatia wa ukanda huo.
Wabunge hao wanatazamiwa kuchunguza kiwango cha uharibifu uliofanywa na hujuma hiyo ya Wazayuni dhidi ya makazi ya raia na majengo yasiyo ya kijeshi na pia kutathmini kiwango cha misaada ya kibinadamu ya kimataifa kwa waathirika wa mashambulio hayo ya kinyama. Wabunge hao vilevile watazungumza na raia wa Palestina walioathirika na mashambulio hayo ya kinyama ya siku 22 na hasa watoto na wanawake.
Mbali na safari ya wabunge hao, wabunge wengine 170 wa bunge hilo la Uingereza wameyakosoa vikali mashirika ya utangazaji ya nchi hiyo BBC na Sky News kwa kutotangaza habari halisi za mashambulio ya utawala wa Israel katika Ukanda wa Gaza na vilevile kukataa kutangaza matangazo ya misaada ya kibinadamu kwa wananchi hao madhlumu. 365265
captcha