IQNA

Mashindano ya kitaifa ya Qur'ani, maalumu kwa wanawake Libya

11:46 - February 18, 2009
Habari ID: 1745468
Mashindano ya kitaifa ya Qur'ani maalumu kwa wanawake yameanza huko Tripoli, mji mkuu wa Libya.
Gazeti la al-Fajr al-Jadid la Libya limeandika kwamba, mashindano hayo yameandaliwa na jumuiya ya masuala ya kheri ya "Wa Itaswimu" ya Libya kwa ushirikiano wa Idara Kuu ya Wakfu na Masuala ya Zaka ya nchi hiyo.
Idadi kadhaa ya viongozi na wawakilishi wa vituo vya Qur'ani, uhifadhi na usomaji wa Qur'ani vya Libya imeshiriki katika sherehe za ufunguzi wa mashindano hayo yanayoendelea katika kituo cha Nur mjini Tripoli.
Wanawake wa Libya wanaoshiriki katika mashindano hayo wanashiriki katika nyanja tatu za kuhifadhi Qur'ani nzima, juzuu 15 za mwisho za Qur'ani na juzuu saba za kitabu hicho kitakatifu.
Mashindano hayo yamepangwa kumalizika kesho Alkhamisi. 365168
captcha