Kituo cha watetezi wa maandishi ya kale ya mkono katika mji wa Shanghai huko kaskazini magharibi mwa China ndicho kilichoandika barua kikitaka nakala ya kale zaidi duniani ya Qur'ani ya maandishi ya mkono kowekwa katika orodha ya taifa ya maandishi ya thamani kubwa na ya kale.
Vitabu vingine vya kale 87 kikiwemo kitabu kitakatifu cha Mabuddha chenye umri wa miaka elfu moja, vimesaliwa katika orodha hiyo ya vitabu vya kale vye thamani nchini China.
Nakala hiyo ya zamani zaidi ya Qur'ani Tukufu yenye umri wa miaka 700 ilipelekwa China kutoka Asia ya Kati na ina juzuu 30 na kurasa 681. Nakala hiyo ya Qur'ani inahifadhiwa katika msikiti mmoja wa mji wa Shanghai. 365759