Kwa mujibu wa gazeti la al-Jazeera, Ali al-Aufi Mkuu wa jumuiya hiyo amesema kuwa, mpango huo ni moja ya njia za kunufaika na teknolojia ya kisasa katika jumuiya na taasisi za Qur'ani. Akisema kuwa jambo hilo ni muhimu sana, al-Aufi amesisitiza kwamba jumuiya zote za Kiislamu na Qur'ani zinapasa kunufaika na teknolojia hiyo kwa maslahi ya Waislamu. Amesema, kutumiwa kompyuta na ratiba zake ni moja ya njia za kusahilisha masuala ya mafunzo, idara na fedha ya jumuiya na vituo vya Qur'ani na kwamba wasimamizi wa vituo hivyo wanapasa kulipa umuhimu suala hilo.
al Aufi ameashiria nafasi ya jumuiya za kuhifadhi Qur'ani katika kuimarisha utamaduni wenye misimamo ya wastani katika jamii na akasema kuwa jumuiya hizo pia zina mchango muhimu katika kuimarisha misimamo ya wastani miongoni mwa watu wenye misimamo ya kupindukia mipaka na vilevile kulinda matakaba ya vijana kutokana na itikadi na fikra potofu.
Amemalizia kwa kusema kwamba, misimamo ya wastani ni katika sunna za Mtume Muhammad (saw) na mafundisho muhimu ya Kiislamu na kwamba walimu na wanafunzi wanapasa kuzingatia jambo hilo. 366755