Kamati ya Vyuo Vikuu vya Palestina nchini Uingereza imetuma barua iliyotiwa saini na zaidi ya wasomi 380 wa vyuo vikuu vya Uingereza kwa wakurugenzi wa majumba ya makumbusho ya London na Manchester ikitaka kufutwa maonyesho ya mafanikio ya kielimu ya vyuo vikuu vya Israel yaliyopangwa kufanyika tarehe tatu na tano Machi.
Miongoni mwa wasomi waliotia saini barua hiyo ni msindi wa tuzo ya amani ya Nobel Mairead Corriga, mwandishi Mmisri Ahdaf Souef, mdhahiri wa Chuo Kikuu cha London Steven Rose, Mwanahistoria mashuhuri wa Uingereza Charles Gink, Baronne Jenny Tong, ambaye ni Msemaji wa chama cha Liberal Democrat katika Baraza la Wazee la Uingereza, na Ian Gabson ambaye ni mbunge wa nchi hiyo.
Sehemu moja ya barua hiyo imesema: Vyuo vikuu saba vya Israel ambavyo vinakusudia kuonyesha mafanikio yao ya kielimu katika majumba ya makumbusho ya Uingereza yalishiriki katika jinai na mauaji ya utawala huo dhidi ya raia wa Gaza kwa kunyamazia kimya jinai hizo. 366734