Akizungumza mjini Qum kusini mwa Tehran, Mandeh Adibzadeh amesema kuwa mashindano ya mwaka huu ya Qur'ani kwa ajili ya wanawake yamefanyiwa mabadiliko na majaji wamepewa uwezo mkubwa zaidi.
Adibzadeh amesema, kwa kuzingatia suala la kuwepo vituo vingi vya kutoa mafunzo ya Qur'ani, kuna haja ya kuwepo taasisi moja ya kuratibu mashindano ya Qur'ani nchini.
Adibzadeh pia ameashiria umuhimu wa kufahamu Qur'an katika maisha ya kila siku. Amesema kuwa kuhifadhi Qur'ani huwa rahisi zaidi iwapo mwenye kuhifadhi anafahamu maana ya aya anazozihifadhi. Amesema kwamba suala hilo litnazidisha kiwango cha ufahamu mbali na kupata thawabu na hivyo kuyafanya maisha ya msomaji yaende kwa mujibu wa mafundisho ya Qur'ani Tukufu.
Adibzadeh amesema, majivuno na kiburi ni moja ya dosari ambazo zinaweza kuwaathiri vibaya wasomaji Qur'ani na kuwapoteza. Amesema, kwa kuzingatia hilo kuna haja kwa Waalimu wa Qur'ani kuwaelekeza na kuwatanabahisha wanafunzi wao wasiwe na tabia ya kiburi na majigambo.
Mandeh Adibzadeh amekumbusha kuwa kutekeleza kivitendo mafunzo ya Quran Tukufu ni muhimu zaidi ya kuhifadi aya zake. Amesisitiza kwamba mbali na kutilia maanani masuala kama vile kusoma na kuhifadhi Qur'ani, kuna haja ya kufahamu na kutekeleza kivitendo miongozo yake katika maisha ya kila siku. 367073