IQNA

Mashindano ya kitaifa ya Qurani kufanyika nchini Qatar

9:04 - February 23, 2009
Habari ID: 1747421
Duru ya kumi na sita ya mashindano ya kuhifadhi Qur'ani Tukufu yanayodhaminiwa na Sheikh Jassim bin Muhammad Aal Thani yameanza leo Jumatatu nchini Qatar.
Mashindano hayo yanafanyika katika Kituo cha Qur'ani cha Arwa bint Abdul Muttalib katika eneo la Dafna.
Gazeti la Qatar la as-Sharq limeandika kuwa sehemu ya kwanza ya mashindano hayo itawajumuisha washiriki 1600 wa vituo vya Qur'ani ambao watagawanywa katika makundi saba. Kuhamasisha Waislamu wahifadhi na kutafakari aya za Qur'ani, juhudi za kuanzisha uhusiano kati ya kizazi kipya cha Waislamu na mafundisho ya Qur'ani na kuhamasishwa moyo wa ushindani salama miongoni mwa washiriki wa mashindano ya Qur'ani ni miongoni mwa malengo ya mashindano hayo ya Qatar.
Malengo mengine ya mashindano hayo yametajwa kuwa ni kusisitiza kuwa matatizo ya kijamii yanaweza kutatuliwa kupitia njia ya kushikamana na Qur'ani na kulea vizazi vinavyozingatia mafundisho ya kitabu hicho cha Mwenyezi Mungu.
Kwa mujibu wa waandaji wa mashindano hayo, mshindi wa kwanza atazawadiwa riali 60,000, wa pili riali 48,000 na wa tatu riali 36'000. 367626
captcha