Waandaji wa warsha hiyo wanasema kuwa lengo lake hasa ni kutafuta njia bora zaidi za kumuarifisha Mtume Muhammad (saw) kwa watu wasiokuwa Waislamu na pia kuandaa uwanja wa kumfahamu zaidi mtukufu huyo.
Zaidi ya wahubiri wa Kiislamu, maimamu wa misikiti na wasimamizi wa vituo vya Kiislamu vya Argentina wapatao 50 wameshiriki katika warsha hiyo.
Ubalozi wa Saudi Arabia mjini Buenos Aires ndio ulioandaa warsha hiyo. 367639