Kwa mujibu wa shirika la habari la Syria SANA, makasisi hao wametoa taarifa wakimtaka Bertholemie, Mkuu wa Baraza la Viongozi wa Makanisa ya Mashariki ya Kati na maimamu wa swala za jamaa wachukue msimamo imara katika kukabiliana na jinai za utawala huo.
Taarifa hiyo imeendelea kusema kuwa, mbali na kutumia silaha zilizopigwa marufuku katika kuwaua kinyama watoto na wanawake wa Ukanda wa Gaza, utawala haramu wa Israel ungali unaendelea na tabia zake za kukanyaga na kudharau matukufu ya kidini na pia kumfanyia dharau Nabii Issa (as) pamoja na mama yake mtakatifu Maryam (as).
Inakumbushwa hapa kuwa, Vatican tayari imekemea kitendo hicho cha Israel na kuitaka iwaombe radhi Wapalestina wa Ukanda wa Gaza kutokana na jinai ulizotenda hivi karibuni dhidi ya wakazi wa eneo hilo. 368278