IQNA

Wanachuo wa Kiislamu Uingereza kukutana Ijumaa ijayo

14:02 - February 24, 2009
Habari ID: 1748191
Wanafunzi wa Kiislamu wa vyuo vikuu vya Uingereza wanatarajiwa kukutana Ijumaa tarehe 27 Februari mjini Tehran. Mkutano huo umeandaliwa na Jumuiya ya Wanafunzi wa Kiislamu Waliohitimu katika Vyuo Vikuu vya Uingereza.
Mkutano huo unafanyika kwa lengo la kuchunguza na kubuni mipango ya mwaka ujao ya jumuiya ya wanafunzi wa Kiislamu waliohitimu masomo katika vyuo vikuu vya Uingereza na kueneza utamaduni wa Kiislamu na Kiirani katika familia zao.
Mkutano huo pia utajadili miongozo ya Kiongozi Muadhamu wa Mapindiuzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei inayosisitiza juu ya udharura wa kuzidishwa maarifa ya Kiislamu ya wanafunzi wa vyuo vikuu kutoka nchi za nje. 368258
captcha