IQNA

Jihadul Islami yalaani uchokozi wa Israel huko Baitul Muqaddas

11:34 - February 25, 2009
Habari ID: 1748286
Kiongozi mmoja wa ngazi za juu wa harakati ya mapambano ya Kiislamu ya Jihadul Islami ya nchini Palestina amelaani hatua za kichokozi za hivi karibuni za utawala haramu wa Israel huko Baitul Muqaddas.
Kwa mujibu wa shirika la habari la Ma'an, Nafidh Azzam, amelaani njama za utawala ghasibu wa Israel za kulifanya eneo hilo takatifu kuwa la Kiyahudi na kudhihirisha wasiwasi na kuchukizwa kwake na hatua ya utawala huo ya kuharibu nyumba 88 na kuwafukuza Wapalestina wapatao 1500.
Amesisitiza kwamba, hujuma zinazotekelezwa hivi sasa na utawala huo dhidi ya Wapalestina huko Baitul Muqaddas, ni utekelezwaji wa njama ambayo ilipangwa miaka mingi iliyopita na utawala huo kwa lengo la kulifanya eneo hilo kuwa la Kiyahudi na kulitenga na ardhi nyinginezo za Wapalestina.
Kiongozi huyo wa Jihadul Islami amesema kuwa, uadui na uchokozi huo wa Wazayuni hautakuwa na natija nyingine isipokuwa kuimarisha zaidi azma ya Wapalestina ya kuungana na kuwa kitu kimoja dhidi ya uchokozi huo.
Nafidh Azzam amewatahadharisha watu wanaokaa kimya kuhusiana na siasa hizo haribifu za Wazayuni wa Israel na kuzitaka jumuiya na mashirika yote ya Kiarabu na ya nchi za Kiislamu kuchukua hatua za haraka za kuunga mkono na kuwalinda Wapalestina dhidi ya uchokozi huo wa Israel, na vilevile kufanya juhudi za kukomboa Baitul Muqaddas na Masjidul Aqsa. 368983
captcha