IQNA

Kufariki dunia Mtume (saw) kulisimamisha wahyi na ufunuo

13:54 - February 25, 2009
Habari ID: 1748567
Kufariki dunia Mtume Muhammad (saw) lilikuwa tukio kubwa duniani ambalo lilipelekea kukatika uhusiano kati ya wahyi na dunia. Tukio hilo la kusikitisha ni miongoni mwamatukio machungu zaidi na yenye hasara kubwa kwa mwanadamu
Kwa hakika kitu cha thamani kubwa zaidi kilichobakishwa na Mtume Muhammad (saw) kwa Waislamu na ambacho kinapaswa kupewa mazingatio maalumu ni Qur'ani Tukufu na Suna za Mtume. Mtume mwenyewe (amani ya Mwenyezi Mungu iwe juu yake na Ali zake) anasema: "Ninawaachia amana ya Qurani hii" na daima alikuwa akiwataka Waislamu kukipa mazingatio maalumu kitabu hicho.
Mtume (saw) alikiwa akisema: Nyumba zetu hazipasi kuwa kama nyumba za Mayahudi na Manasara. Amesema: "Zitieni nyumba zenu nuru kwa kusoma Qur'ani."
Vilevile thawabu nyingi zilizotajwa kwa ajili ya kusoma Qur'ani ni ishara kwamba Mtume Muhammad (saw) alikuwa akiuhamasisha umma kusoma Qur'ani mara kwa mara na kukifanya Qur'ani kuwa kitabu cha maisha ya kila siku.
Mtume Muhammad (saw) alifariki dunia tarehe 28 Safar mwaka 11Hijria. 369043


captcha