IQNA

Waislamu wote wanawapenda Ahlul Bait na Imam Hussein (as)

10:38 - February 26, 2009
Habari ID: 1748778
Sheikh Maulawi Muhibbi ambaye ni miongoni mwa maulama wa Ahlusunna nchini Iran amesema kuwa Waislamu wote Washia kwa Wasuni, wanawapenda Ahlubaiti wa Mtume Muhammad (saw).
Sheikh Maulawi ameutaja Uislamu kuwa ni dini ya jihadi huku akiashiria vita vya jihadi vya Mtume (saw) mjini Madina. Amesema kuwa Imam Hussein, mjukuu wa Mtume (saw) alielewa kwamba iwapo mapambano ya jihadi yatazimwa dini ya Mwenyezi Mungu pia itatoweka na kwa msingi huo alijitolea muhanga ili kuzibadilisha nyoyo za wanadamu.
Sheikh Maulawi Muhibbi amesema kuwa Imam Hussein (as) ni safina ya uongofu na kwamba Waislamu wote Shia na Suni, wanawapenda Watu wa Nyumba Tukufu ya Mtume Muhammad (saw). Amesisitiza kuwa Imam Hussein alijitoa muhanga yeye na jamaa zake kwa ajili ya kuhuisha dini ya Mwenyezi Mungu na Suna za Mtume Muhammad (saw) na kwa msingi huo ana nafasi makhsusi katika nyoyo za Waislamu wote. 369396

captcha