Hayo yamesemwa na Brigedia Ali Fadhli kamanda wa kikosi kilichotajwa huko Kashan na kuongeza kuwa, mapambano na ukakamavu unaoonekana nchini Iran, vita vya siku 33 nchini Lebanon na vya siku 22 dhidi ya adui Mzayuni katika Ukanda wa Gaza, yote hayo yanatokana na utamaduni wa mapambano ya Imam Ali na Imam Hussein (as) dhidi ya maadui wa Uislamu. Amesema, Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran ni matokeo ya juhudi na mapambano ya muda mrefu ya miongo kadhaa ya Imam Khomeini (MA), marjaa na wanazuoni wengine wa kidini ambao walihisi kuwa na majukumu mazito katika kukabiliana na maadui wa Uislamu.
Brigedia Ali Fadhli amesema, mchango uliotolewa na wapiganaji wa Kiislamu katika vita vya kujitetea kutakatifu vya Iraq dhidi ya Iran hauna mfano wake katika historia. 369831