Mwandishi wa IQNA nchini Pakistan amesema kuwa mwandishi wa tarjumi hiyo Sheikh Taqi Uthman amekuwa akifunza tafsiri ya Qur’ani, hadithi na fiqhi kwa miaka mingi katika kituo cha Darul Ulum mjini Karachi.
Mwandishi wa tarjumi hiyo amezingatia zaidi suala la kutumia lugha nyepesi na rahisi ili kuwafaidish zaidi watu kawaida. Vilevile amejaribu kutumia istilahi zinazofahamika na watu wote na kujiepusha na maneno na istilahi ngumu.
Tarjumi mpya ya Qur’ani tukufu kwa lugha ya Kiurdu imechapishwa katika juzuu tatu. 369617