Maonyesho hayo yatakayoendelea kwa muda wa siku tatu yanawashirikisha wataalamu 20 wa mimea iliyotajwa na Qur'ani pamoja na maudhui tofauti za bustani na shamba katika Qur'ani. Wataalamu hao ni kutoka nchi kama vile Malaysia, Pakistan, Misri, Palestina, Morocco, nchi wanachama wa Baraza la Ushirikiano la Ghuba ya Uajemi, Marekani, Malaysia na Indonesia.
Halima Bint Ali, Waziri wa Elimu ya Juu wa Malaysia ni miongoni mwa watu waliopangiwa kuzungumza katika mkutano huo.
Mimea katika Qur'ani, hadithi za Mtume (saw) na elimu mpya, mazingira na kuhifadhiwa kwake katika mtazamo wa Kiislamu, sanaa ya Kiislamu, uchoraji na maendeleo pamoja na usanifu majengo wa Kiislamu ni miongoni mwa mambo yatakayojadiliwa katika mkutano huo. 370111