IQNA

Isesco yalaani dharau ya televisheni ya Israel dhidi ya Mtume wa Uislamu

10:49 - March 01, 2009
Habari ID: 1749653
Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Jumuiya ya Nchi za Kiislamu, Isesco, limelaani vikali hatua ya dharau ya televisheni moja ya utawala haramu wa Isreal dhidi ya Mtume Mtukufu (saw).
Shirika la Isesco limetoa taarifa likilaani vikali hatua hiyo ya kanali ya kumi ya televisheni ya utawala haramu wa Israel ya kudharau na kumkosea heshima Mtume Mtukufu (saw). Limesema, dharau hiyo ni alama ya wazi ya mielekeo ya ubaguzi wa rangi na uadui wa utawala huo dhidi ya Uislamu na Waislamu.
Imeendelea kusema kuwa, hatua hiyo pia inathibitisha unyama na siasa za mabavu za Uzayuni katika jumuiya za kimataifa na dhidi ya thamani za kidini.
Hivi karibuni kanali hiyo ya televisheni ya utawala wa Kizayuni ilidharau matukufu ya Waislamu kwa kumtusi Mtume Muhammad (saw), Nabii Issa na mama yake mtakatifu (as), hatua ambayo tokea wakati huo imekuwa ikilaaniwa vikali na jumuiya za kimataifa pamoja na baadhi ya nchi za Kiislamu.
Isesco vilevile imezitaka nchi za dunia kutokaa kimya kuhusiana na hatua za dharau za utawala haramu wa Israel dhidi ya matukufu ya dini za mbinguni ukiwemo Uislamu, pamoja na nembo za kidini za Waislamu na Wakristo. 370234
captcha