IQNA

Uislamu Waarifishia Waislamu chakula halali kupitia Qur'ani

10:58 - March 02, 2009
Habari ID: 1750215
Dini tukufu ya Kiislamu imewausia Waislamu kula baadhi ya vyakula na vinywaji na kuzingatia mfumo maalumu wa kula kupitia mafundisho ya Qur'ani. Wakati huohuo, imewataka Waislamu kujiepusha kabisa na baadhi ya vyakula na vinywaji vyenye madhara kwao.
Akizungumzia suala hilo katika mahojiano na waandishi wa Shirika la Kimataifa la Habari za Qur'ani IQNA, Minai, mtafiti na mtaalamu wa mafundisho ya Qur'ani kuhusiana na masuala ya tiba ya Kiislamu amesema kwamba kitabu hiki kitakatifu kimetaja wazi baadhi ya wanyama halali wanaopasa kuliwa nyama yao na wale haramu wanaopasa kuepukwa na Waislamu kutokan na madhara yao kwa mwili na roho ya mwanadamu.
Ameashiria aya zinazozungumzia nyama halali inayopasa kuliwa na Waislamu kuwa ni aya 21 ya Suratul Waqia, Baqara aya 57, A'raaf aya 160, Taha aya 80 na Maida aya 97. Minai amesema kuwa katika aya ya 149 ya Suratul Baqarah, Mwenyezi Mungu ameweka wazi kwamba ni chakula kisafi tu ndicho kinachopasa kuliwa na Waislamu na kuwazuia waja wake wasile chakula kichafu na haramu kilicho na madhara kwao.
Mtafiti huyo wa masuala ya Qur'ani amesema, mfumo maalumu wa ulaji chakula katika Uislamu unatimia kupitia ushauri wa mafundisho ya Kiislamu wa kuwataka wafuasi wake wale chakula kwa kipimo cha kumtosheleza mtu na sio kula kupita kiasi hadi mtu kuvimbiwa au kufanya israfu katika utumiaji wa chakula. 370566
captcha