IQNA

Kanali ya televisheni ya Kiislamu yaanzishwa nchini Mauritius

10:46 - March 02, 2009
Habari ID: 1750403
Waislamu wa Mauritius wameanzisha kanali ya televisheni ya satalaiti itakayokuwa ikirusha hewani vipindi vya Kiislamu katika maeneo mbalimbali ya dunia.
Vipindi cha televisheini hiyo vinajumuisha hotuba za maulamaa wa Kiislamu, mashindano ya Qur'ani, hadithi na maisha ya masahaba wa Mtume Muhammad (saw). Televisheni hiyo pia inatayarisha vipindi vya mafunzo ya Kiislamu.
Televisheni hiyo vilevile inafundisha watazamaji wake mbinu za kisasa za kusoma na kuhifadhi Qur'ani, lugha ya Kiarabu na tajwidi. 370967

captcha