IQNA

Kuanza wiki ya "Ujue Uislamu" huko Colorado, Marekani

15:51 - March 03, 2009
Habari ID: 1751231
Wiki ya "Ujue Uislamu" ilianza juzi katika Chuo Kikuu cha Colorado huko Marekani. Shughuli hiyo imetayarishwa na Jumuiya ya Wanachuo wa Kiislamu wa chuo hicho.
Gazeti la Colorado Daily limeandika kuwa lengo la shughuli hiyo ni kuiarifisha dini na utamaduni wa Kiislamu kwa njia sahihi kwa wasiokuwa Waislamu na kuwasaidia katika kuelewa vyema mafundisho ya dini hiyo.
Moja ya ratiba za wiki ya Ujue Uislamu ni hotuba ya mwandishi maarufu wa Kiislamu Ridha Aslan ambaye atazungumzia suala la kukabiliana na propaganda chafu zinazofanywa dhidi ya Uislamu.
Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Colorado nchini Marekani ambao wanafanya jitihada za kusahihisha sura isiyokuwa sahihi inayotangazwa dhidi ya Uislamu na Waislamu, wametayarisha ratiba nyingine kadhaa katika kipindi cha wiki nzima ya tamasha ya wiki ya Ujue Uislamu. 371588

captcha