Mwandishi wa IQNA nchini Syria ameripoti kuwa katika wiki hii kumetayarishwa ratiba mbalimbali ikiwa ni pamoja na matamasha ya mashairi, filamu na hotuba za wasomi kuhusu ushindi wa wananapambano wa Palestina dhidi ya Wazayuni wa Israel huko Gaza.
Muhammad Nizal ambaye ni mwanachama wa Idara ya Kisiasa ya Hamas amesema katika sherehe za ufunguzi wa wiki ya "Gaza Imeshinda" kwamba Hamas itafanya jitihada za kukomboa mateka wote wa Kipalestina wanaoshikiliwa katika korokoro za utawala wa Kizayuni wa Israel.
Muhammad Nizal amesema, Hamas haitofautishi kati ya mateka wa Kipalestina wanaoshikiliwa na Israel na kwamba lengo lake kubwa ni kukomboa Wapalestina wote bila ya kujali mielekeo yao ya kisiasa.
Amesisitiza kuwa harakati ya mapambano ya Wapalestina inakabiliwa na hujuma za kisiasa na ya vyombo vya habari ambazo ni kali zaidi ya hujuma za kijeshi na kwamba utawala ghasibu wa Israel unataka kufikia malengo ambayo umeshindwa kupata katika mashambulizi ya kijeshi dhidi ya raia wa Ukanda wa Gaza kwa kutumia hujuma za kisiasa na propaganda za vyombo vya habari. 372959