Moja ya ramani za wasanii hao zilizokubaliwa katika maonyesho hayo ni ya kujengwa Taasisi ya Kiutamaduni ya Kiislamu ambayo matawi mawili yake yatakuwa katika barabara kuu za Stephenson na Polonceau.
Mkuu wa maonyesho hayo amesema kuwa ramani za majengo ambazo zimewasilishwa katika maonyesho hayo zinatofautiana sana, jambo ambalo limezingatiwa sana na marefa wa maonyesho hayo.
Kundi la Lyon ambalo limeshinda tenda ya ujenzi wa taasisi hiyo hadi sasa limewasilisha ramani za ujenzi wa majengo katika miji mingi ya Ufaransa ukiwemo mji mkuu, Paris. 373613