Mwandishi wa IQNA katika eneo la kusini mwa Asia ameripoti kuwa mtalii huyo wa Kiirani hadi sasa amekwishatembelea nchi 28 duniani katika safari hiyo.
Ismail Salehabadi anasema kuwa lengo lake ni kulingania amani na uvumilivu wa dini ya Kiislamu na kujifunza tamaduni za mataifa mengine.
Kuhusu natija ya safari yake hadi sasa Salehabadi anasema, karibu asilimia 95 ya watu wote duniani wana ada na desturi zinazofanana za kimaisha. 373643