IQNA

Abdulhussein Khosropanah: Hakuna mgongano baina ya dini ya sayansi

13:29 - March 08, 2009
Habari ID: 1753178
Historia ya fikra za Kiislamu inaonyesha kuwa hakuna mgongano baina ya dini ya sayansi katika ulimwengu wa Kiislamu kama ilivyokuwa katika nchi za Magharibi; kwani changamoto nyingi katika ulimwengu wa Magharibi zilitokana na misimamo isiyokuwa sahihi na ya kuchupa mipaka ya kanisa na fikra zake finyu na zisizokuwa na mantiki dhidi ya wanasayandi na wasomi.
Hayo yamesemwa na Hujjatul Islam Walmuslimin Abdulhussein Khosropanah Naibu Mkuu wa Kituo cha Utafiti cha Utamaduni na Fikra za Kiislamu nchini Iran na kuongeza kuwa uchambuzi na uchunguzi wa uhusiano wa sayansi na dini una umuhimu mkubwa hususan kwa wanafalfasa, kwani uvumbuzi wa uhusiano au utengano kati ya vitu hivyo viwili utasaidia mno ustawi wa maarifa ya dini na sayansi na hatimaye kuweka wazi ukweli wa mambo.
Sheikh Khosropanah amesema kuwa, mivutano iliyotokea katika karne zilizopita kati ya sayansi na dini inaonyesha umuhimu wa mjadala huu. Amesema kuwa japokuwa mivutano hiyo iliikumba dini ya Kikristo na Biblia lakini baadhi ya mafanikio ya kisayansi yametoa changamoto kwa itikadi za kidini za dini mbalimbali kama vile mjadala juu ya kuumbwa na kukamilika kwa mwanadamu ambao unadai, chanzo na asili ya mwanadamu si udongo bali na mnyama mithili ya mwanadamu. 374123

captcha