IQNA

Ayatullah Nury Hamedani:

Tuko tayari kufanya mdahalo na Mawahabi

16:15 - March 10, 2009
Habari ID: 1754420
Ayatullahil Udhmaa Nury Hamedani ambaye ni miongoni mwa wanazuoni wakubwa wa Kiislamu katika mji mtakatifu wa Qum nchini Iran ametoa changamoto kwa Mawahabi kuketi kwenye meza ya mdahalo.
Ayatullah Hamedani ameashiria mkutano wa kuwaunga mkono wananchi wanaodhulumiwa wa Palestina uliofanyika hivi karibuni mjini Tehran na akasema kuwa Iran imethibitisha kwamba ndiye mtetezi mkuu wa watu wanaokandamizwa na inachukizwa na madhalimu.
Amesema kuwa hotuba ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran Ayatullah Ali Khamenei na kuhudhuria kwake katika mkutano huo kumetoa tahadhari kwa nchi mbalimbali duniani na kudhihirisha zaidi suala la mauaji ya kizazi yanayofanywa na Wazayuni huko Palestina.
Kuhusu suala la mdahalo na Mawahabi, Ayatullah Hamedani amesema kuwa mdahalo umepewa nafasi maalumu katika dini ya Kiislamu na kwamba amekuwa akiwataka Mawahabi kuketi kwenye meza ya mdahalo na kwamba yuko tayari kufanya mdahalo na kundi hilo.
Mwanazuoni huyo mkubwa wa kidini amesema, iwapo Mawahabi wana dalili za wanayofanya wanapaswa kukubali kufanya mdahalo. 375121

captcha