Katika sherehe iliyoanza kwenye msikiti wa Wangzi Ying imam wa msikiti huo amewahutubia Waislamu akieleza sira ya Mtume Muhammad (saw) kwa mujibu wa aya za Qurani Tukufu na akawahamasisha Waislamu kufuata akhlaki njema na mwenendo wa Mtume huyo wa Mwenyezi Mungu.
Sherehe hiyo pia ilihutubiwa na Mkuu wa Kitengo cha Utamaduni cha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran mjini Peking ambaye amewapa mkono na baraka Waislamu wote kwa mnasaba wa kuwadia siku za kuzaliwa Nabii wa rehma Muhammad (saw).
Muhammad Jawad Aghajeri amesema kuwa kuna mpango wa kuanzisha masomo ya Qur'ani katika msikiti huo na akapendekeza kutumwa makarii wa Kiirani katika msikiti huo kwa ajili ya kutoa mafunzo ya Qur'ani.
Vile vile amemtunuku Imam wa Msikiti wa Wangzi Ying mjini Peking nakala kadhaa za vitabu vya sira ya Mtume na kitabu cha hadithi cha Mizanul Hikma.
375235