Kwa mujibu wa shirika la habari la Kuwait KUNA, kikao hicho cha siku mbili kinachochunguza matunda ya fikra za Kiislamu kimeandaliwa na Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kiislamu ya Kuwait na kwa usimamizi wa Nawaf Ahmad al-Jabir Swabah, Mriti wa Kiti cha Ufalme wa nchi hiyo.
Washiriki wa kikao hicho watachunguza njia za kuimarisha mazungumzo kati ya Japan na ulimwengu wa Kiislamu katika mitazamo mbalimbali.
Kikao hicho kilichoanza saa tatu kimehudhuriwa na Hussein Nassir al-Hureiti, Waziri wa Wakfu na Masuala ya Kiislamu wa Kuwait. 376529