Maneno hayo yamesemwa na Bi Ashrat Batul, msomaji wa kimataifa wa Qur'ani katika mahojiano yake na Iqna ambaye ameshiriki katika kikao cha 14 cha kimatifa cha Qur'ani na Hadfithi kilichoandaliwa na Taasisi ya Kimataifa ya al-Mustafa (saw).
Batul amesema kuwa, duru hii ya mashindano hayo ya kimataifa imezishinda duru nyingine zilizopita za mashindano hayo kwa kutilia maanani kwamba, ubora wake umeimarishwa zaidi na kiwango cha washiriki katika mashindano hayo pia kimeboreshwa.
Akielezea sababu ya kuvutiwa kwake na kisomo cha Abdul Basit, Bi Batul amesema kuwa jambo hilo linatokana na ukweli kwamba wakati anaposoma Qur'ani huwa anazingatia maana ya kina ya kitabu hicho kitakatifu na kuiakisi kwa uwezo wake wote ili kumnufaisha msikilizaji wake. Amesema kuwa jambo hilo linapasa kuzingatiwa na wasomaji wote wa Qur'ani kwa sababu msomaji hapasi kuzingatia tu sauti nzuri ya usomaji Qur'ani bali anapasa kuipa umuhimu maana ya aya anazosoma.
Bi Batul amesema kuwa maana ya aya za Qur'ani ni muhimu kuliko sauti inayotolewa wakati wa kusoma aya hizo, na kuongeza kwamba, wasomaji wote mashuhuri wa Qur'ani huzingatia vyema jambo hilo. 376251