Kwa mujibu wa shirikal habari la Ma', wanafunzi wa kike na kiume walioshiriki katika mashindano hayo walishindana katika kuhifadhi Qur'ani nzima, juzuu tatu, juzuu mbili na juzuu moja ya kitabu hicho cha Wahyi wa Mwenyezi Mungu.
Nuha Shatat, mkuu wa idara iliyotajwa amesema lengo la kufanyika mashindano hayo ni kuimarisha moyo wa mashindano salama na vipawa vya Qur'ani miongoni mwa wanafunzi. Akisisitiza kwamba kuhifadhi Qur'ani kuna nafasi muhimu katika kuimarisha vipawa vya wanafunzi, Shatat amesema kuwa takwimu zinaonyesha wazi kuwa katika miaka iliyopita, wanafunzi waliofanya vyema katika masomo yao ni wale waliohifadhi Qur'ani Tukufu.
Akibainisha kuwa kuhifadhi Qur'ani kuna athari nyingi hapa duniani na huko Akhera, amewataka Wapalestina kuwasaidia watoto wao katika jukumu la kihifadhi na kusoma kitabu hicho kitakatifu.
Viongozi wa idara hiyo ya malezi na mafunzo wameelezea mshangao na kufurahishwa kwao na kuvutiwa idadi kubwa ya wanafunzi wa Ukanda wa Gaza kuhusiana na suala la usomaji na uhifadhi wa Qur'ani Tukufu katika miaka ya hivi karibuni na kuwatakia kila la kheri katika majukumu yao ya kila siku maishani. 377428