IQNA

Kuanza kikao cha kimataifa cha Fiqhi ya Kiislamu nchini Uturuki

11:27 - March 14, 2009
Habari ID: 1755622
Kikao cha kimataifa cha Fiqhi ya Kiislamu kilichoandaliwa na Jumuiya ya Kimataifa ya Fiqhi ya Kiislamu kilianza siku ya Alkhamisi huko Istanbul nchini Uturuki.
Kwa mujibu wa tovuti ya Muhit, kikao hicho ambacho kinafanyika chini ya anwani ya 'Fiqhi ya Kiislamu na Changamoto za Zama', kinahudhuriwa na wanazuoni, wanafikra na wasomi zaidi ya 40 wa Kishia na Kisuni kutoka nchi mbalimbali za dunia. Haki za kiraia katika fiqhi ya Kiislamu, demokrasia na haki za binadamu, haki za mwanamke katika fiqhi ya Kiislamu, fiqhi ya Kiislamu na mila na ukisasa ni miongoni mwa maudhui muhimu zitakazojadiliwa katika kikao hicho.
Akizungumza katika kikao cha ufunguzi, Abu al-Qassim Dibaji, Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Fiqhi ya Kiislamu amesisitiza juu ya umuhimu wa kusawazishwa kwa misimamo ya Kiislamu na kufunguliwa milango ya mazungumzo na nchi za Magharibi.
Washiriki wa kikao hicho vilevile wametahadharisha dhidi ya siasa za nchi za Magharibi za kuwalenga kwa makusudi wanawake wa Kiislamu kwa madhumuni ya kuharibu mfumo wa familia na kudhoofisha misingi ya kidini ya jamii za Waislamu duniani. 377465
captcha